Ili uwe wa kwanza kupata machapisho yetu kila siku usisahau
kubonyeza button ya follow kulike na kukoment . na kama unaswali zaid
ruhusa kuuliza kupitia kiboksi hapo chini
. ahsaante
Faida 6 Za Ukwaju Katika Urembo,Afya Na Nywele
Wengi wetu ni wapenzi wa juice ya hili tunda na wengi
tunaitumia majumbani kupunguza uzito, lakini kumbe ukwaju una matumizi mengi
tofauti tofauti ukianzia kwenye afya, urembo na hata nywele.
Katika Ngozi husaidia
- Kungarisha ngozi
- kuondoa weusi kwenye shingo
- hutibu chunusi
Katika Nywele husaidia
- Kuzuia Kukatika Kwa Nywele
- Husaidia kutibu ngozi ya kichwa yenye mafuta
Katika Afya Ukwaju
- unasaidia kupunguza uzito
Jinsi ambavyo unaweza kutumia ukwaju kwa ajili ya ngozi
kungarisha ngozi
mahitaji
- tunda za ukwaju – 30 grams ( robo kilo)
- maji ya moto – 150 grams ( chupa mbili za George weah/drop
kubwa)
- manjano – nusu kijiko cha chai
Namna ya kufanya
- loweka tunda za ukwaju katika maji ya moto kwa dakika
kumi
- toa mbegu na ubaki na juice nzito ya ukwaju
- ongeza manjano katika juice hio ya ukwaju\
- paka mchanganyiko wako katika uso wako na uache kwa
dakika 15
- osha kwa maji ya vuguvugu
Note – mchanganyiko huu unasaidia zaidi kwa wenye sura/nyuso
zenye mafuta unaweza kufanya hivi mara mbili kwa week.
Kuondoa weusi kwenye shingo
Mahitaji
- juice ya ukwaju nzito – kijiko kimoja
- asali – kijiko kimoja
- rose water ( maji ya mawardi)–
kijiko kimoja
Namna Ya Kufanya
- changanya juice ya ukwaju, rose water na asali
- paka mchanganyiko huu katika shingo na uuache kwa dakika 20
- osha shingo yako kwa rose water au maji ya uvuguvugu
Fanya hivi mara moj kwa wiki katika kipindi cha miezi miwili
utaona matokeo
Kutibu chunusi
Mahitaji
Matumizi
- changanya mahitaji yako ( mtindi, ukwaju na manjano)
- paka usoni na ukae nao mpaka ukauke, unaweza kuchukua
dk 20-30
- osha uso kwa maji ya vuguvugu na paka mafuta kwa ajili
ya ku moisturize ngozi
Fanya hivi mara mbili kwa wiki sio tu itaondoa chunusi bali
pia itakupa ngozi nyororo
Ukwaju Katika Nywele
Kuzuia ukatikaji wa nywele
Mahitaji
- 15 gram za ukwaju ( ukwaju robo ugawe mara nne)
Matumizi
- loweka ukwaju wako katika maji acha kwa dakika 10
- toa mbegu na upate juice ya ukwaju, paka katika nywele
na ngozi ya nywele massage kwa dakika kadhaa ( si zaid ya 10)
- tumbukiza taulo katika maji ya moto na ukamue kidogo
- tumia taulo hili kufunga kichwa chako kikiwa bado kina
mchanganyiko huo, acha mchanganyiko huu kwa nusu saa.
- osha mchanganyiko wako kwa shampoo ukifuatiwa na
conditioner
fanya hivi mara mbili kwa week kuzuia kukatika kwa nywele
Husaidia kutibu ngozi ya kichwa yenye mafuta( mba)
ngozi yenye mafuta inaweza kusababisha matatizo mengi kwenye
nywele ikiwepo m’ba na kukatika
kwa nywele
Mahitaji
- juice ya ukwaju (nzito) – vijiko viwili
- olive oil –
kijiko kimoja
- butter milk – kijiko kimoja
Matumizi
- changanya juice ya ukwaju,olive oil na butter milk
- paka mchanganyiko wako katika nywele na umassage kwa
muda wa dk 5-10
- acha mchanganyiko wako ukae kwa dakika 15, kama utakua
unakukera vaa mfuko wa plastic
- osha kwa kutumia maji ya vuguvugu na shampoo
rudia kufanya hivi mara mbili kwa wiki kuondoa mafuta katika
ngozi ya nywele zako.
unasaidia kupunguza uzito
Mahitaji
- Ukwaju na maji
Matumizi
- unaweza kutengeneza kama juice ama kuwa una weka ukwaju
katika maji yako ya kunywa
- kutumia kinywaji hichi mara mbili kwa siku unaweza
kupungua uzito kwa haraka, masaa matatu baada ya kula na muda wa kulala
Note: Ukwaju una uwezo mkubwa wa kupunguza mwili, usitumie
kinywaji hiki kama huna mwili mkubwa sana na kama una vidonda vya tumbo.
Ili uwe wa kwanza kupata machapisho yetu kila siku usisahau
kubonyeza button ya follow kulike na kukoment . na kama unaswali zaid
ruhusa kuuliza kupitia kiboksi hapo chini
. ahsaante
0 Comments