SABABU ZA BARKAH KATIKA NYUMBA
‘’Na lau kwamba watu wa mji(nyumba)
wangeamini na kumcha mungu tungeliwafungulia
juu yao Baraka kutoka mbinguni na ardhin’’
1. Bismillah na kumtaja allah
amesema rasulu llah (s.a.w)’’anapoingia mmoja
wenu katika nyumba basi na amtaje allah (s.w)
wakati anapoingia na wakati
anapokula,husema shetwani kumwambia mtu
huyo sitakuja mchana wala usiku’’
2. Kuswali swala kwa wakati
Amesema allah (s.w)’’na uamrishe watu wako
kuswali na wawe na subra nayo hatuta kuuliza
rizki kwani sisi tutakuruzuku na mwisho mwema
kwa wamchao mungu’’.
3. Kusoma qur-an tukufu
Amesema rasulu llah (s.a.w)’’someni surat
bakrah kwani kuisoma kwake ni Baraka na
kuiacha kwake ni khasara na wala
hatoihifadhi mnafiki’’
4.kumcha mungu
Amesema allah (s.w) ‘’ ’Na lau kwamba watu wa
mji(nyumba) wangeamini na kumcha mungu
tungeliwafungulia juu yao Baraka kutoka mbinguni
na ardhin na lakini wamekanusha tukayachukua
waliyokua nayo kwa yale muliyoyachuma kwa
mikono yenu’’
5.kula chakula kwa pamoja
Amesema rasulullah (s.a.w)’’kuleni kwa pamoja na
wala musitengane kwani barka hupatikana kwa
kula pamoja,chakula cha mmoja hutosha
wawili,chakula cha wawili hutosha watatu na
wanne’’
6.kutafuta riski mapema(asubuhi mapema)
Amesema rasulullah(s.a.w)’’barka za ummati
wangu zipo katika kutafuta riski kwa
mapema’’(yaani kutoka mapema kuelekea kutafuta
riski).
7.kumtegemea allah kikweli
Amesema rasulullah(s.a.w)’’ lau kama
mtamtegemea allah kiukweli atakuruzukuni kama
anavyowaruzuku ndege hutoka asubuhi matumbo
matupu na akirudi ameshiba’’
8. kuwa wakweli wakati wa manunuzi na mauzaji
Amesema rasulullah ‘’uzianeni kwa kheir bila kuleta
mtafaruko,kwani ukweli huleta barka katika
mauziano na uongo huondosha barka’’
9.sadaka
Miongoni mwa sababu za barka katika nyumba ni
kutoa sadaka hasa hasa kutoa kwa siri kwani
hupunguza ghadhabu za mungu
10.kuswali kwa pamoja mume na mke kwa upole
Amesema rasulullah’’kwa anaetaka kufunguliwa
riski na aswali kwa upole.’’
11.kushukuru sana kwa kila jambo
Amesema allah(s.w)’’ na lau kama mtanishukuru
basi nitawazidishieni’’
12.kukithirisha sana na kudumu na istighfaru
Amesema rasulullah (s.a.w)’’yeyote ataye dumu na
istighfaru allah atamjalia wepesi kila penye ziki na
humpa faraja kila panapotatizo na humruzuku rizki
bila kipimo’’.
~~~~~~~~~wallah aalamu~~~~~~~~~~
Kitabu hiki ni sadaka kwa ajili ya marehemu baba
yangu na afya njema kwa familia yangu ni ruhusa
kutoa kopi na kueneza kwa waislam wengine kwa
lengo la kupata barka kutoka kwa allah.
Namuomba allah atuwafikishe katika mambo ya
kheir.
please eneza link hii ili wengine iwafikie iwe sadaka kwangu na kwako pia.
0 Comments