Subscribe Us

header ads

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

 

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA



USISAHA KUSUBSCRIBE KUKOMENT NA KULIKE PAGE HII ILI UWE WA MWANZO KUPATA MAKALA ZETU ZA KILA SIKU. AHSANTE.

Nimekua nikipata maswali wengi juu ya faida za majani ya miti tofauti ikiwemo ile ambayo inatuzunguka kila siku, kwa iyo leo naleta faida za majani ya mpera na makala nyengine nitaleta faida za pera lenyewe

1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi,

1.   Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy)

2.   Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini na hivyo kupunguza uzito

3.   Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini ni nzuri kwa wagonjwa wa sukari

4.   Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume kwani inasaidia kuamsha hisia na kupitisha damu katika mishipa midogo ya uume jambo ambalo litasababisha uume kua imara na wenye nguvu.

5.   Pia inatumika kama scrub ya uso chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni

6.   Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara
8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yaliyoshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria yaani tetnus
9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong’atwa na mdudu na kupunguza maumivu
10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume
11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu chunusi ,saga majani ya mpera tia na maji ya uvuguvugu halafu paka usoni kaa kwa dakika 10-15 osha uso wako
12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza uzito mwilini na kuzuia kupata magonjwa hatarishi kama kisukari na presha.
13. Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako
14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi, maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera na utaona maajabu ya majani haya
15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi inayoanza kuzeeka mapema
16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu mvurugiko wa tumbo.
Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibu maradhi mbalimbali , halikadhalika juisi ya mapera nayo husaidia sana kutibu mgolo au bawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katika moyo.
Kimsingi mti wa mpera karibu kila sehemu yake ni tiba kwani hata mizizi yake inapochemshwa na kutumia kwa kunywa huenda kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya hedhi au wenye matatizo ya kutokwa na maji yenye harufu mbaya sehemu zao za siri.
Sanjari na hayo, watoto wadogo wenye matatizo ya kutopata choo zaidi ya siku mbili, wakinyweshwa maji ya majani hayo baada ya kuchemshwa huwasaidia kuondokana na shida hiyo.

 

USISAHA KUSUBSCRIBE KUKOMENT NA KULIKE PAGE HII ILI UWE WA MWANZO KUPATA MAKALA ZETU ZA KILA SIKU. AHSANTE.

                       Share na wengine wanufaike

 

Post a Comment

0 Comments