Subscribe Us

header ads

Njia nane za kuboresha uwezo wa ubongo wako

 




Njia nane za kuboresha uwezo wa ubongo wako

Umeshajipata katika hali ambapo unajaribu bila mafanikio kukumbuka jina la mtu au kitu fulani au mahala fulani lakini huwezi kukumbuka kabisa?

Mara nyingi tunaambiwa kuwa uwezo wa kukumbuka unapungua wakati mtu anazidi kuwa mzee.

Lakini kuna matumaini kuwa kuna njia za kuboresha ubongo wetu.

Kwa hivyo kama unataka kuboresha uwezo wa ubongo wako basi kuwa tayari kufanya mambo haya.

1. Mazoezi hufanya ubongo wako kuwa mkubwa

Ni kweli ubongo wetu huwa mkubwa wakati tunafanya mazoezi.

Mazoezi huchangia ubongo kuwa na mawasiliano mazuri na pia huchangia seli zaidi kukua.

Kama unafanyia mazoezi yako nje basi inakuwa bora kwa sababu utakuwa na manufaa zaidi ya kupata vitamini D

Fanyia mazoezi katika mazingira mapya na njia mpya za kufanya mambo mengine.

2. Kariri vitu ukiendelea na shughuli zingine.

Hii ni mbinu ambayo pia imetumiwa na wacheza filamu: kama unajaribu kukariri maneno fulani au kujaribu kujifunza kitu huku ukitembea tembea, unaweza kushika kwa njia rahisi kile unachokariri.

Ikiwa wakati mwingine utakuwa labda na hotuba ya kukariri, mbona usitembetembe au ucheze densi kukusaidia kushika kwa njia rahi kile unachokifanya.

3. Kula chakula kinachosaidia kukua kwa ubongo.

Karibu asilimia 20 ya sukari au chakula cha kutupa nguvu unachokula kinaelekea kwa ubongo, na kuufanya ubongo kutegemea sana sukari.

Ikiwa viwango vya sukari haviwezi kudhibitiwa akili yako itahisi kuchanganyikiwa. Ukila chakula unachokipenda hutoa kemikali inayojulikana kama dopamine kwa eneo fulani la ubongo na ndio maana unahisi vizuri ukila chakula hicho.

Seli za ubongo hujengwa kwa mafuta, kwa hivyo ni muhimu kutotoa mafuta kutoka kwa chakula chako. Mafuta kutoka kwa njugu, nafaka , parachichi na samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo.

4. Kupumzika.

Misongo mingine ya mawazo ni muhimu kwa sabubu inatuwezesha kuchukua hatua za haraka wakati dharura: huchangia homoni kwa jina cortisol na wakati ikipasuka hutuwezesha kupata nguvu na kufanya jamba kwa umakini.

Lakini msongo wa muda mrefu huathiri sana ubongo.

Kwa hivyo ni muhimiu kujua kuwa tunastahili kupumzika mara moja kwa wakati fulani kuwezesha pia ubongo kupumzika.

5. Tafuta njia zingine za kujipa changamoto.

Njia muhimu ya kuboresha ubongo wako ni kuuoa changamoto kwa kujifunza kitu kipya kabisa.

Shughuli kwa mfano kujifunza kuchora au kujifunza lugha mpya huchangia ubongo kuboreka zaidi.

Unaweza pia kucheza michezo ya mitandaoni dhidi ya marafiki au watu wa familia.

6. Sikiliza Muziki

Ushahidi unaonyesha kuwa muziki huboresha ubongo kwa njia ya kipekee

Wakati ukingalia ubongo wa mtu ambaye anasikiliza muziki au anayecheza muziki ni kuwa ubongo wote hushiriki.

Jiunge na kikundi na waimbaji au lipa tiketi kuhudhuria tamasha la bendi unayoipenda.

7. Somea mtihani kitandani

Kama utajifunza kitu kipta wakati wa mchana, huwa kunatokea mawasiliano kati ya seli moja ya ubongo na nyingine

Unapolala, mawasiliano huwa dhabiti na huwa unakumbukakile umejifunza.

Kwa hivyo kulala ni kitu muhimu katika kujikumbusha kile umesoma.

Ikiw unampa mtu kitu cha kujifunza kabla hajalala, watakikumbuka wanapoamka asubuhi kuliko kumpa mtu kitu cha kukariri mapema asubuhi.

Ikiwa unasomea mtihani, jaribu kupitia maswali na majibu kichwani mwako wakati unakaribia kulala.

8. Amka vizuri

Sote tunaju kuwa kulala ni kitu muhimu, chini ya saa tano za kulala hautafikiria vizuri, huku kulala zaidi ya saa kumi utahisi umechoka.

Lakini jambo ku litakalokuwezeha kufanya vyema siku nzima ni jinsi utaamka.

Lala kwenye chumba chennye giza na amka ukiongeza mwangaza taratibu.

Mwangaza huu hupitia kwenye macho yaliyofungwa na kuujulisha ubongo ili kuamsha homoni inayoitwa cortisol.

Kiwango cha homoni ya cortisol mwilini mwako wakati unapoamka huathiri jinsi ubongo wako utafanya kazi siku hiyo.

 

Post a Comment

1 Comments