Subscribe Us

header ads

ufahamu


UFAHAMU
Ufahamu ni uwezo wa kuelewa jambo fulani na kuweza kulifafanua.
AINA ZA UFAHAMU
  1. Ufahamu wa kusoma
  1. Ufahamu wa kusikiliza
  1. Ufahamu wa kutafakari
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
- Ni kuzingatia yote yasemwayo na mtu mmoja, mwingine kusikiliza kunahitaji umakini na utulivu ili kuelewa.
- Watu huweza kupata taarifa kutokana na kusikiliza jambo husika kwa umakini na utulivu
Mfano: -
Mtoto akimsikiliza mwalimu kwa umakini huweza kufanya vizuri kwenye masomo. Hiyo kutokana na kumsikiliza mtu unaweza kupata maarifa, taarifa za kufurahisha/kuhuzunisha.
UFAHAMU KUHUSU KICHOCHO
Kichocho ni ugonjwa hatari sana , vilevile kichocho ni hatari katika jamii kiujumla. Pia kichocho kinaathiri wakubwa na watoto hasa wale wenye umri chini ya miaka 5,6 na 7.
Pia ugonjwa wa kichocho hutokana kwa njia mbalimbali ikiwemo kukojoa kwenye maji machafu, maji taka (mifereji)
UFAHAMU WA KUSOMA
Kusoma ni uwezo wa kuelewa maneno yaliyoandikwa. Ufahamu wa kusoma umegawanyika katika makundi mawili
  • Kusoma kimya
  • Kusoma kwa sauti
Msomaji anaweza kusoma kwa kutumia njia moja kati ya hizo mbili lengo ni kuelewa jambo au ujumbe aliosoma.
Katika kusoma mtu anaweza kupata maarifa/ ujumbe mbalimbali wa kufundisha au kuhuzunisha na hata msisimuko kutokana na yaliyosomwa.
DHIMA ZA UFAHAMU
  1. Husaidia katika kuokoa muda
  1. Husaidia katika kupunguza gharama
  1. Husaidia kutoa taarifa kwa ufupi na kumwezesha mtu kufuata maagizo.
  1. Husaidia sana kukuza, kuelewa miongoni mwa wanafunzi.
      5. Huelimisha.
UFUPISHO WA HABARI
Ni hali ya kusoma au kusikiliza habari na hatimaye kuiandika au kusimulia kwa ufupi bila kupoteza maana yake ya msingi.
Ni kitendo cha kuelewa habari uliyosoma au kusikiliza kwa kifupi kwa kutumia maneno yako mwenyewe. Msomaji huchukua mawazo makuu ya habari aliyonayo kulinganisha pamoja na mawazo yake mwenyewe.
LENGO LA UFUPISHO WA HABARI
  1. Ufupisho hutumika katika shughuli za kila siku
  1. Husaidia katika kupata kuelewa na usikivu (msomaji, msikilizaji)
  1. Hurahisisha habari hivyo kuokoa muda
  1. Hutumika katika kuandaa ripoti mbalimbali.
  1. Husaidia kudondoa hoja mbalimbali zinazotokana na hotuba na mihadhara.
MFANO WA HABARI
Baba na mama wanajishughulisha zaidi na masuala ya kilimo. Mazao ambayo hupanda ni kama vile mahindi, mtama, ulezi, uwele n.k
UFUPISHO WAKE
Wazazi wangu ni wakulima wa mazao ya nafaka.
ZOEZI
Fupisha habari ifuatayo kwa maneno yasiyopungua....
Tatizo la kweli la kidunia ya leo si umaskini kwa maana tunao ujuzi wa mali zinazotuwezesha kufuta umaskini huo. Tatizo lenyewe hasa ni mgawanyiko wa binadamu katika tabaka mbili: -
o   Tabaka la mahitaji
o   Tabaka la umaskini
Jambo hili ndilo linaloleta tatizo la vita na chuki kati ya watu.
UFUPISHO WAKE
Tatizo la tabaka mbili, tabaka la mahitaji na tabaka la umaskini.



Post a Comment

0 Comments