UANDISHI WA INSHA
TARATIBU ZA UANDISHI
Alama na mpangilio wa maneno ni
mojawapo ya vigezo vya kutambulisha mwandishi bora hodari kaziiwezekuwa nzuri
inayoeleweka na wasomaji, mwandishi hana budi kutumia mfumo wa alama ili
kumsaidia msomaji wapi pa kumpumzisha, kuuliza swali n.k baadhiya alama
zifuatazo hutumika katika uandishi.
Mkato (,)
Alama hii hutumika
- kuweka pumziko fupi
katika sentensi
- kutenga maneno yaliyo
katika orodha
- huonyesha sehemu mbili
za sentensi zilizo kinyume
Mfano: - Umoja ni nguvu,
utengano ni dhaifu
NUKTA (.)
Alama hii hutumika
- kukamilisha sentensi
- kuonyesha ufupisho wa
maneno
mfano: - R.T.D (Radio Tanzania
Dar es salaam)
NUKTA MKATO (;)
Alama hii hutumika
Kuunga sentensi mbili
zinazoweza kusimama zenyewe bila kutumia kiunganishi.
Mfano: -Hapo zamani za kale
wazee walijiheshimi; sikuhizi hawajiheshimu.
Humpa msomaji pumziko fupi
katika sentensi.
NUKTA/ NUKTA PACHA(:)
Alama hii hutumika
- kuunga sentensi mbili
zinazoweza kusema zenyewe, bila kutumia kiunganishi
- kuunga/kuonesha vitu
vilivyo katika orodha
mfano: - Nilileta vitu hivi:
wino, karatasi, embe, ndizi na nanasi.
ALAMA YA MSHANGAO (!)
- Hutumika baada ya neno
au usemi wa kushangaza au kushtuka
- Hutumika kuonesha
msisitizo, kushangaa, kero n.k.
Mfano: - Hivi ni kweli! Mwone
alivyo.
ALAMA YA KUULIZA (?)
Huonesha hali ya kuuliza swali
katika tungo/ sentensi
Mfano: -
- Wanakuja saa ngapi?
- Wanamaana gani?
MABANO [ ( ) ]
Hutumika kuonesha maana ya
ziada katika sentensi
Mfano: - Nchi yangu (Tanzania)
naipenda sana
KISTARI (-)
Hutumika kuunda maneno
Mfano: - Ed-elfitr,
Dar-es-salaam
Hutumika badala ya nukta mbili
Mfano: - tulipofika mbugani –
tuliwaona swala wamelala – Swala dume na watoto watatu.
- Hutumika kuonesha kama neno
limekatwa kwa kuwa limefika ukingoni.
ALAMA ZA MTAJO (“ ”)
Hutumika kuonesha maneno
yaliyosemwa na mtu mwingine katika sentensi.
Mfano: - Nguchiro alisema “
hakika mzee Ngwale ni katili sana”
Hutumika kubainisha maneno ya
kigeni katika lugha nyingine.
Mfano: - (“ yes” )
katika kiswahili.
UANDISHI WA INSHA
UANDISHI WA INSHA
Insha ni kifungu cha habari chenye
kueleza hoja au picha za mtu juu ya jambo fulani
- Insha hugawanywa katika
vifungu, navyo ni: -
- Insha huweza kuwa na haya
moja au wakili na kila haya hubeba wazo kuu moja matumizi
- Kuna aina kuu mbili za insha
(i) Insha za wasifu
(ii) Insha za hoja
INSHA
HIKI NI KIELELEZO CHA ISHA ZA HOJA NA WASIFU
HIKI NI KIELELEZO CHA ISHA ZA HOJA NA WASIFU
INSHA ZA WASIFU
|
INSHA ZA HOJA
|
-
Insha za wasifu za kisanaa
-
Insha za wasifu zisizo za kisanaa.
|
-
Insha za hoja
-
Insha za kisanaa
-
Insha za hoja zisizo za kisanaa
-
Insha za wasifu
|
INSHA ZA HOJA
Hueleza mawazo fulani na hupanga
mengine
Mifano ya vichwa vya insha
vifuatavyo ni vya insha ya hoja.
-
Elimu itolewe kwa watoto wa kiume tu.
-
Shule za kutwa ni bora kuliko shule za bweni.
INSHA ZA WASIFU
Hii hueleza sifa za watu au vitu
kama wanyama, milima, miti au mahali fulani: -
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANDISHI
WA INSHA
- KICHWA CHA INSHA
Huandikwa kwa herufi
kubwa katikati juu ya insha
Huandikwa kwa ufasaha na kwa
muhtasari
Kichwa kisizidi maneno
matano(5)
- MWANZO WA INSHA
Huzingatia tafsiri ya jambo
linalozungumzwa, uhusiano wake na vitu vingine.
Kwa kawaida mwanzo huzidi aya
moja
- KIINI CHA INSHA
Hii ni sehemu kuu ya insha
huzingatia mawazo makuu ambayo hupangwa katika haya zenye mtiririko mzuri wa
mawazo.
Hueleza kwa undani juu ya
jambo linalozungumzwa kwa uthibitisho.
- MWISHO WA INSHA
Hutoa
msisitizo kwa yaliyojadiliwa
Huonesha muhtasari wa
yaliyojadiliwa na kuandikwa pamoja na hitimisho.
MAMBO YANAYOHITAJIKA KATIKA UTUNGAJI WA INSHA
1. Kichwa cha habari chenye kueleweka
MAMBO YANAYOHITAJIKA KATIKA UTUNGAJI WA INSHA
1. Kichwa cha habari chenye kueleweka
- Kuandika kwa kufuata kanuni na taratibu za uandishi
- Kutumia lugha fasaha na rahisi.
- Andika mwisho wa insha unaowavutia wasomaji au
wasikilizaji.
INSHA KUHUSU MISITU
MISITU
Mimi naitwa Ajazi Mohamed natokea
kijiji cha Njoro kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro. Katika kijiji hicho naishi
na babu pamoja na bibi alikadhalika na ndugu zangu. Kila ifikapo jumamosi mimi
na ndugu zangu huwa tunakwenda kukata kuni pia kuchuma matunda kama mananasi,
maembe, machungwa pia maparachichi. Misitu husaidia kwa ajili ya kivuli,
mvua pamoja na kuni. Pia misitu hiyo hiyo hutoa mbao kwa ajili ya kutengenezea
vifaa vya nyumbani vikiwemo, meza, viti, makabati pamoja na vitanda. Pia mbao
hutumika kujenga mapaa ya nyumba na kadhalika.
Misitu hiyohiyo hupenda kukaa
wanyama wakali kama vile mbwa mwitu, nyoka na wadudu wenye sumu wakiwemo
nyuki,dondola. Misitu ipo sehemu mbalimbali ikiwemo Moshi, Arusha, Songea
pamoja na Singida. Misitu ni hatari sana hasa kwa watoto wadogo kwenda peke yao
msituni au mwanamke kutembea peke yake jioni au usiku huwa ni hatari sana kwa
sababu msituni kuna wanyama wakali sana na unaweza kukutana na majambazi.
Misitu ni muhimu kwa ajili ya
mahitaji yetu ya nchi na ya nyumbani kwa ujumla pia tunasisitiza kutunza
misitu, mazingira na maeneo tunayoishi.
TOFAUTI KATI YA INSHA ZA KISANAA NA ZISIZO ZA KISANAA
Insha za kisanaa
- Hizi ni Insha ambazo hutumia vipengele mbalimbali vya kifasihi katika kuwasilisha ujumbe. Mbinu hizo ni kama vile Nahau, Methali, Misemo, Tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa.
Insha zisizo za kisanaa
- Hizi ni Insha ambazo hazitumii lugha ya kifasihi katika kufikisha ujumbe wake.
TOFAUTI KATI YA INSHA ZA KISANAA NA ZISIZO ZA KISANAA
Insha za kisanaa
- Hizi ni Insha ambazo hutumia vipengele mbalimbali vya kifasihi katika kuwasilisha ujumbe. Mbinu hizo ni kama vile Nahau, Methali, Misemo, Tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa.
Insha zisizo za kisanaa
- Hizi ni Insha ambazo hazitumii lugha ya kifasihi katika kufikisha ujumbe wake.
0 Comments