UANDISHI WA BARUA
BARUA
Ni maandishi yenye ujumbe
yanayopelekwa kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali
Mfano wa njia hizo ni: -
- Posta
- Mkono
- Basi au ndege n.k
Kuna aina mbalimbali za barua kama
vile: -
- Barua za kirafiki
- Barua rasmi
- Barua za mialiko
- Barua za kindugu
BARUA ZA KIRAFIKI
Hizi ni barua ziandikwazo kwa
marafiki, jamaa, ndugu, wazazi.
LENGO LA BARUA ZA KIRAFIKI
- Kusalimiana na ndugu zetu
- Kuomba msaada
- Kutoa pongezi, hongera au pole
- Kuomba msamaha
MUUNDO WA BARUA ZA KIRAFIKI
Barua za kirafiki huundwa na mambo
muhimu yafuatayo
- Anuani ya mwandishi
- Tarehe
- Mwanzo wa barua
- Mwisho wa barua
- Jina la mwandishi.
(i) ANUANI YA MWANDISHI
-
Huandikwa juu kwenye pembe ya kulia ya karatasi. Huandikwa kwa waziwazi na kwa
usahihi ili mwandikiwa aitumie kujibu barua aliyotumiwa
-
Huweza kuandikwa kwa muundo wa mshazari au wima.
MFANO WA MSHAZARI
SHULE YA SEKONDARI MAKONGO
S. L.P
60157
DAR ES SALAAM
19/07/2012
MFANO WA WIMA
SHULE YA SEKONDARI MAKONGO
S. L.P 60157
DAR ES SALAAM
19/07/2012
(ii) TAREHE
-
Huandikwa chini kwenye anuani ya mwandishi ili kumjulisha mwandikiwa lini barua
imeandikwa
-
Tarehe huweza kuandikwa kwa miundo mbalimbali mfano: - 2-02-2012, 02/02/2012,
2.2.2012 au february
(iii) MWANZO WA BARUA
Huandikwa kushoto chini ya mstari wa
tarehe huweza kuandikwa kwa kutajwa jina, eneo au wadhifa wa mtu anayeandikiwa
Mfano: -
Mpendwa Baba, mama, kaka, mpenzi
wangu na pia sehemu hii kukaa maneno ya sehemu maamkizi ili kujulikana kati ya
mwandishi na mwandikiwa
(iv) KIINI CHA BARUA
Sehemu hii hueleza kusudi/lengo la
mwandishi, huelezea kusudi lake la kuandika barua.
Mfano: -
- Kuomba kazi
- Kuomba msaada
- Kuomba msamaha
- Kujuliana hali
(v) MWISHO WA BARUA
Hapa huwa na salamu za maagano na
salamu hizo kutegemea mwandishi na mwandikiwa, mwisho wa barua huwa na maneno
yenye ladha na mvuto.
Mfano: -
Wasalamu/
nisalimie wote wanaonifahamu nakusubiri kwa hamu n.k
(vi) JINA LA
MWANDISHI
Ni muhimu mwandishi kuandika jina
ili kumjulisha mwandikiwa barua imetoka kwa nani.
Angalizo: -
Uandishi wa barua za kirafiki hufuata taratibu zote za uandishi
Mfano:-
- Mkato
- Nukta
- Alama za kuuliza
- Mshangao n.k
SHULE
YA SEKONDARI MAKONGO
S.
L.P 60157
DAR ES SALAAM
19/07/2012
Baba mpendwa;
Salamu sana, je! Hamjambo wote hapo
nyumbani? Wale mbuzi wangu mapacha niliowaacha wamezaa tena? Natumaini wadogo
zangu kulwa na doto wanaendelea vema na masomo.
Dhima la barua hii ni kutaka kukujulisha
maendeleo yangu ya shuleni ya kidato cha kwanza. Pia tatizo kubwa
linaloniandama hapa shuleni ni umaskini sina hata shilingi moja ya kununua hata
kipande cha mboga. Hivyo naomba nitumie hela ya matumizi ili nisome vizuri.
Wasalimie wote hapo nyumbani pamoja
na marafiki zangu wote.
Wako akupendaye
ELIMUKAZI
0 Comments