MAWASILIANO
LUGHA
Lugha ni nini?
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu
zenye kubeba maana zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika
mawasiliano.
-
Lugha ndio nyenzo kuu ya mawasiliano baina ya binadamu na binadamu.
-
Kimsingi lugha hutumia sauti zenye maneno ambayo yamepangiliwa kwa njia maalumu
ili kuleta maana iliyo kusudiwa.
-
Binadamu hutumia lugha ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku, watu hutumia
lugha kupashana habari, kubadilisha mawazo.
- Ili
mawasiliano yawepo, mpangilio wa maneno huna budi kuleta maana.
-
Lugha hutofautiana kulingana na watumiaji.
Mfano:
o Kihaya ni lugha
inayotumika na wahaya
o Kibena ni lugha
inayotumika na wabena
o Kijerumani ni lugha
inayotumika na wajerumani
Lugha hujengwa kwa maneno, maneno
hujengwa kwa vitamkwa vyenye mpangilio maalum ambao hulipa neno maana. Maneno
yakipangwa kwa njia maalum hutoa kauli zenye maana.
Hivyo lugha ili iweze kuleta
mawasiliano baina ya wazungumzaji muundo wake huanzia vitamkwa, maneno na hata
kauli hupangiliwa kwa njia maalum.
Mfano:
Vitamkwa: - chu, ch, k,a,l,u,o
vitamkwa hivi hujenga maneno- chakula, chuo nk.
Katika lugha ya kiswahili vitamkwa
hukamilishwa kwa kutumia herufi za alfabeti. Alfabet zimegawanyika katika
konsonati na irabu
Konsonati: -
b,c,d,f,g,h,j,k,l,m,n,p,q,r,s,t,v,w,x,y,z.
Irabu: -a,e,i,o,u
Kutokana na alfabeti hizi lugha ya
kiswahili imejenga maneno mbalimbali ambayo ndio msingi wa mawasiliano kwa
watanzania na mataifa mengine.
- Mawasiliano yasiyotumia
sauti sio lugha kwa sababu hapo hutumii sauti wala maneno vilevile mawasiliano
ya wanyama, wadudu hayawezi kuitwa lugha kwa sababu hiyohiyo.
LUGHA FASAHA
Ni lugha ambayo inafuata taratibu
zote za lugha hiyo yaani , kimaana, kimuundo kimatamshi na kimantiki.
Ili mawasiliano yawe mazuri, wazungumzaji watumie lugha
fasaha.
(a) Maana: -
Ili lugha iwe fasaha katika misingi ya maana au msamiati
uliokusudiwa, mfano neno barabara lina maana mbili. Mtu anaweza kukosea badala
ya kusema njia akasema sawasawa.
(b) Muundo: -
Ufasaha wa lugha hujitokeza kutokana
na mpangilio wa maneno kuwa mzuri,
Mfano: - kikubwa kitabu badala ya kitabu kikubwa
(c) Matamshi: -
Sauti za lugha yoyote ile zitamkwe
kama zinavyotakiwa ili kujenga ufasaha katika lugha hiyo.
Mfano baadhi ya watu hushidwa kutamka
baadhi ya maneno
Mfano: zambi badala ya dhambi
Zarura badala ya
dharura
(d) Mantiki
Ili maana iliyolengwa iweze kuwepo
kauli lazima ziwe na mantiki
Mfano: Nimemkuta hayupo badala
ya sijamkuta
Chai imeingia nzi badala ya inzi ameingia kwenye chai
ATHARI ZA KUTOTUMIA LUGHA FASAHA
Lugha isipotumika kwa ufasaha
(i) Yaweza kukwamisha mawasiliano
(ii) Lugha hiyo kukosa hadhi na
kuonekana kama ya wahuni
0 Comments