FASIHI KWA UJUMLA
Fasihi:
Ni sanaa inayotumia lugha ili
kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa .
Ni sanaa kwa sababu huumbwa kwa
lugha katika hali ya kuvutia na kuweka madoido ya kila namna ili iweze kuvutia
wasomaji au wasimuliaji wake, lengo lake kuu ni kufikisha ujumbe kwa jamii.
SANAA
Ni uzuri unaojitokeza katika umbo
lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisia zinazomgusa kwa kutoa
kielelezo chenye maana. Hivyo unaona kazi za sanaa katika nyanja mbalimbali
kama vile: -
- Utarizi
- Fasihi
- Ushonaji
- Muziki
- Ususi
- Ufumaji uchoraji
DHIMA ZA FASIHI
(i) Kusisimua
(ii) Kuhifadhi na kurithisha
amali za jamii
(iii) Kudumisha na kuendeleza lugha
(iv) Kuelimisha jamii
(a) KUSISIMUA
Hujikita zaidi katika mpangilio wa
maneno lugha ya picha mandhari, tamathali au semi
Mfano: -
Ndugu yetu ametutupa mkono
(amefariki)
Sentensi inajaribu kutuliza uchungu
na hivyo kuleta faraja.
(b) Kuhifadhi na kurithisha
amali za jamii
Fasihi huhifadhi na kutunza mila na
desturi za fani na pia huweza kurithisha mila hizo kutoka kizazi kimoja hadi
kingine.
(c) Kudumisha na kuendeleza
lugha
Kwa kadri lugha inavyotumiwa na
watumizi, maneno yalivyobuniwa na kuenezwa zamani, leo yanatumiwa na watunzi wa
mashairi, kwaya , nyimbo n.k
(d) Kuelimisha jamii
Fasihi hukosoa, huonya na
kurekebisha jamii hueleza waziwazi wale wanaotenda kinyume na matakwa ya jamii,
inabidi kukemea na kuonyana kwa kutumia methali, nahau
Mfano: - Asiyesikia la mkuu
huvunjika guu
Hii inatoa tahadhari
AINA ZA FASIHI
Kuna aina mbili (2) za fasihi
(a) Fasihi andishi
(b) Fasihi simulizi
- FASIHI SIMULIZI
Ni fasihi ambayo hutumia masimulizi
ya mdomo kufikisha ujumbe wake kwa jamii.
Ni fasihi ambayo ni kongwe na
ilianza tangu binadamu alipoanza kuishi duniani.
FASIHI SIMULIZI INA TANZU NNE NAZO
NI
(i) Hadithi
(ii) Semi
(iii) Ushairi
(iv) Maigizo
2. FASIHI ANDISHI
Ni fasihi ambayo hutumia maandishi
ili kufikisha ujumbe kwa jamii
Fasihi andishi ina tanzu nne
(i) Tamthilia
(ii) Ushairi
(iii) Ngonjera
(iv) Riwaya
TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA
FASIHI ANDISHI
NA
|
FASIHI SIMULIZI
|
FASIHI ANDISHI
|
1
|
Huwasilishwa na fanani kwa njia ya
masimulizi au mdomo
|
Huwasilishwa kwa maandishi kwa
njia ya maandishi
|
2
|
Huifadhiwa kichwani na kusambazwa
na mdomo au mazungumzo
|
Huifadhiwa kwa maandishi na
kusambazwa kwa maandishi
|
3
|
Huruhusu mabadiliko ya papo kwa
papo
|
Hairuhusu mabadiliko ya papohapo
kazi ikishaandikwa haibadiliki hadi toleo jingine
|
4
|
Ina tanzu nne kama vile
-
Hadithi
-
Semi
-
Sanaa za maonesho maigizo
|
Ina tanzu tatu kama vile
-
Ushairi
-
Tamthilia
-
Riwaya
|
5.
|
Hadhira yake ni watu wale katika
jamii
-
Watoto
-
Wazee
-
Wasomi
|
Hadhira yake ni watu wale wanaojua
kusoma na kuandika
|
6
|
Inaumri mkubwa
|
Ina umri mdogo imekuwepo baada ya
ugunduzi wa maandishi
|
7
|
Ni rahisi kusahau baadhi ya
vipengele
|
Si rahisi kusahauliwa baadhi ya
vipengele kwani imehifadhiwa kwa maandishi.
|
8
|
Muundo wake ni wa moja kwa moja
|
Mara nyingi muundo wake ni wa mchangamano
unaruhusu urejeshi
|
9
|
Huenda na wakati na mabadiliko ya
matukio katika jamii
|
Haiendi na wakati kwa sababu
ikishaandikwa haiwezi kubadilishwa.
|
TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi hujitokeza katika
tanzu kuu nne, ambazo ni hadithi, semi, ushairi, na maigizo. Tanzu hizi
zinaweza kuoneshwa katika mchoro ufuatao na vipera vyake
HADITHI
Ni tungo za fasihi simulizi
zitumiazo lugha ya ujazo na maongezi ya kila siku.
Masimulizi huwa ni mafupi
yaliyopangwa katika mtiririko unaokamilisha visa.
VIPERA VYA HADITHI
(i) Ngano
(ii) Tarihi
(iii) Vigano
(iv) Soga
NGANO
Hizi ni hadithi zitumiazo wahusika
kama wanyama, miti na watu kuelezea au kuonya.
TARIHI
Ni hadithi ambazo husimulia kuhusu
matukio ya kihistoria, matukio hayo yanaweza kuwa ya kweli au ya kubuni.
VIGANO
Ni hadithi fupi zinazoelezea makosa
au uovu wa watu fulani na kueleza maadili yanayofaa. Vigano hutumia methali
kama msingi wa maadili yake.
SOGA
Ni hadithi fupi za kuchekesha na
kukejeli. Wahusika wa soga ni watu wa kubuni. Soga husema ukweli unaohimiza
lakini ukweli huo hujenga vichekesho ili kupunguza makali.
USHAIRI
Ushairi katika fasihi simulizi ni
fungu linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo ya sauti kwa utaratibu
maalumu
VIPERA VYA USHAIRI
(i) Mashairi
(ii) Utenzi
(iii) Nyimbo
(iv) Ngonjera
MASHAIRI
Ni tungo zenye mpangilio maalumu wa
silabi na lugha ya mkato.
UTENZI
Ni tungo ndefu ya kimasimulizi au
kimawaidha utenzi kutofautiana na ushauri kwa kuwa na mistari mifupimifupi
isiyozidi mizani.
NYIMBO
Ni tungo zenye mpangilio maalumu wa
maneno na mahadhi yaani hupenda kuimbwa na kuambatana na ala za muziki au
sanaa.
NGONJERA
Zina muundo wa mashahiri ya
kimapokeo na huwa katika muundo wa mazungumzo baina ya watu wawili au makundi
ya watu wanaolumbana na mwishowe kufikia mwafaka/ suluhisho.
SEMI
Ni tungo za fasihi simulizi ambazo
ni fupi na zenye kutumia lugha ya picha.
VIPERA VYA SEMI
(i) Methali
(ii) Mafumbo
(iii) Nahau
(iv) Vitendawili
METHALI
Ni misemo ambayo hutoa hekima na
busara kwa kuundwa kwa mpangilio wa pande mbili za fikra
Mfano: -
- Kidole kimoja hakivunji
chawa
- Haba na haba hujaza kibaba
MAFUMBO
Ni kauli zinazoeleza maana waziwazi
na kutumia maficho
Mfano:-
- Hakamatiki hashikiki (moshi)
- Uzalendo umemshinda (
umeshindwa kuvumilia)
KITENDAWILI
Ni usemi uliofumbwa hutolewa kwa
hadhira, ufumbuliwe, kitendawili kufanya kazi ya kumfikisha msikilizaji.
Mfano: -
Uzi mwembamba umefunga dume
(usingizi)
NAHAU
Ni kauli zilizojengwa kwa picha kwa
kutumia maneno ya kawaida lakini zinatoa maana isiyo ya kawaida.
Mfano: -
-
Amepata jiko (ameoa)
- Ana
mkono mrefu (mwizi)
- Ana
mkono wa birika (mchoyo)
-
Amevaa miwani (amelewa)
MAIGIZO SANAA ZA MAONYESHO
Ni masimulizi yenye utendaji ambayo
huonesha mambo yaliyotokea, yatakayotokea lengo ni kufikisha ujumbe.
VIPERA VYAKE NI:-
(i) Michezo ya kuigiza
(ii) Majigambo
(iii) Ngonjera
(iv) Vichekesho
MICHEZO YA KUIGIZA
Ni maigizo marafu ya visa
vinavyowakilisha maisha ya jamii fulani. Michezo mingine huafiki na mingine
hulaani mambo yasiyofaa, michezo ya watoto wadogo pia huwasaidia kujifunza
maadili ya jamii hiyo.
MAJIGAMBO
Ni maigizo ya kujitapa /kujigamba
kutokana na kuweza kufanya jambo la kishujaa au lisilo la kawaida. Mtambaji
husimulia na kutenda akionyesha jinsi alivyofanya jambo lile.
Mfano: -
Askari aliyerudi vitani,mtu
aliyemuua simba n.k
NGONJERA
Ni maigizo ya kutumia mashairi, huwa
kuna pande mbili unapinga na unaelewa jambo na mwisho kufikia muafaka.
VICHEKESHO
Ni maigizo mafupi ya kufurahisha
hadhira
Mfano: -
- Mizengwe
- Original komedi
- Vituko show
FANI NA MAUDHUI
Kazi ya fasihi lazima iwe na fani na
maudhui, vipengele hivi ni sura za falsafa moja si rahisi kuzitenganisha fani
imo ndani ya maudhui.
FANI
Ni umbo la nje la kazi ya fasihi
MAUDHUI
Ni jambo analosema muandishi katika
kazi yake ya fasihi
VIPENGELE VYA FANI
(i) Matumizi ya lugha
(ii) Mtindo
(iii) Muundo
(iv) Mandhari au
mazingira
(v) Wahusika
(vi) Jina la kitabu.
MATUMIZI YA LUGHA
Msanii hutoa lugha kwa mpangilio
maalumu wa maneno, tamathali za semi hutumiwa kwa upekee kulingana na mahitaji
ya kazi hiyo.
MTINDO
Hii ni tabia ya pekee mtunzi katika
simulizi au uandishi mtindo kutofautiana hali ya mtunzi na mtunzi.
MADHARI
Ni sura ya mahali mazingira ambapo
kazi ya fasihi husika
WAHUSIKA
Ni watu, miti au viumbe hai
vinavyowakilisha watendaji katika kuonyesha sifa za ndani na nje.
VIPENGELE VYA MAUDHUI
Kuna vipengele (5) vya maudhui navyo
ni
(i) Dhamira
(ii) Ujumbe
(iii) Falsafa
(iv) Migogoro
(v) Mafunzo
DHAMIRA
Ni lengo la mtunzi wa kazi za
fasihi. Mtunzi anaweza kutoa dhamira kuu na kujenga dhamira ndogondogo dhamira
huweza kukosoa.
UJUMBE
Ni funzo analotoa mtunzi katika kazi
ya fasihi kulingana na dhamira alizotoa
FALSAFA
Ni mawazo makuu ya mtunzi kuhusu
maisha. Ni imani ya maandishi kuhusu maisha.
MIGOGORO
Ni hali ya kutoelewa na baina ya
pande mbili au zaidi.
MAFUNZO
Ni mafunzo makuu ya mtunzi kuhusu
maisha.wakati mwingine hadhira inaweza kupata mafunzo mabaya au mazuri kwa
wahusika wakazi hiyo.
UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
Maana;
Uhakiki ni kazi au kitendo cha kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi.
au
Uhakiki ni sayansi maalum ya kuchambua kazi ya sanaa kwa undani na kuona ubora wa kazi ya fasihi kwa kutumia vipengele vya fani na maudhui na kuangalia uwiano na uhusiano wake na jamii.
UMUHIMU WA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
1. Kuchambua na kuweka wazi fumbo ambalo litapatikana na kazi ya fasihi.
2. Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi.
3. Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora.
4. Kumuelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila dira ya muhakikiki (mhakiki ni mwalimu wa jamii)
5. Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
6. Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji.
7. Kutafuta na kuweka sawa nadharia ya vitabu teule.
KUFAFANUA VIGEZO VYA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI.
1. Ukweli wa mambo yanayoelezwa.
2. Uhalisikaji wa watu, mazingira na matukio katika jamii.
3. Umuhimu wa kazi ya fasihi kwa jamii inayohusika lazima ufikiriwe.
UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI KATIKA FANI.
Maana;
Uhakiki ni kazi au kitendo cha kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi.
au
Uhakiki ni sayansi maalum ya kuchambua kazi ya sanaa kwa undani na kuona ubora wa kazi ya fasihi kwa kutumia vipengele vya fani na maudhui na kuangalia uwiano na uhusiano wake na jamii.
UMUHIMU WA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
1. Kuchambua na kuweka wazi fumbo ambalo litapatikana na kazi ya fasihi.
2. Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi.
3. Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora.
4. Kumuelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila dira ya muhakikiki (mhakiki ni mwalimu wa jamii)
5. Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
6. Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji.
7. Kutafuta na kuweka sawa nadharia ya vitabu teule.
KUFAFANUA VIGEZO VYA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI.
1. Ukweli wa mambo yanayoelezwa.
2. Uhalisikaji wa watu, mazingira na matukio katika jamii.
3. Umuhimu wa kazi ya fasihi kwa jamii inayohusika lazima ufikiriwe.
UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI KATIKA FANI.
- Wahusika
- Mandhari
- Mtindo
MAUDHUI
- Ujumbe
- Mtindo
ZOEZI
- Fasihi ni nini
Fasihi ni sanaa inayotumia lugha ili
kufikisha ujumbe kwa jamii fulani iliyokusudiwa
- Orodhesha vipera vinne (4) vya semi na mfano
(i) Methali (kidole kimoja
hakivunji chawa)
(ii) Mafumbo ( uzalendo
umemshinda)
(iii) Nahau (amepata jiko) –
Ameoa
(iv) Vitendawili (uzi mwembamba
umefunga dume) – Usingizi
- Ainisha aina za maneno katika sentensi hii
Paka wale weusi walikuwa wanatembea
ovyo barabarani
W
TS
T
E
- Taja matumizi mawili ya herufi kubwaa
(i) Hutumika kuandika jina, mahali
ili kuleta maana .Mfano wa majina Asha, Ally Mfano wa mahali, Dar es salaam,
Tanga n.k.
(ii) Hutumika mwanzo wa sentensi
0 Comments