Subscribe Us

header ads

usimulizi wa hadithi


USIMULIZI WA HADITHI
Usimulizi wa hadithi ni hali ya kueleza kitu au kuhadithia hadithi kwa njia ya mdomo.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA USIMULIZI WA HADITHI
(i) Kutumia lugha fasaha
(ii)  Kuzingatia kiimbo
(iii)  Matamshi
(iv) Mtiririko wa matukio ili walengwa waweze kuelewa kinachosimuliwa.
(v)  Vitendo na maigizo ili kukwepa kuwachosha wasikilizaji
MASIMULIZI YA HADITHI
Ni masimulizi yenye lugha ya mjazo na mtiririko wake huwa sahihi au rahisi mara nyingi masimulizi ya hadithi huwa mafupi. Usimulizi ,utazamaji wa hadithi huwa na sifa kadhaa. Kinachotambulisha sifa hizo ni sehemu ya ambayo haiwezi kupotea au kupata pindi tusomapo kitabu.
Moja sauti ya mtambaji, msimulizi huusika moja kwa moja kwa hadithi
Utendaji wake jukwaani una nafasi kubwa ya hadhira. Utendaji huenda sambamba na lugha.
SIFA ZA UTENDAJI SIMULIZI
(i) Usemi halisi
(ii) Urudiaji
(iii) Sauti igizi
(iv) Matumizi ya viashiria
(v)  Matumizi ya wakati
(vi)  Uigizaji
  1. USEMI HALISI
Msimulizi anasema moja kwa moja hadhira waweze kuelewa kwa urahisi na wasichoke kusikiliza.
  1. URUDIAJI
Kama vipengele vingi vinavyorudiwa kama vile maneno, vifungu, nyimbo n.k
  1. SAUTI IGIZI
Msimulizi anaweza kuiga sauti fulani kwa kutumia lugha inayomwezesha kubadilisha sauti yake katika fani mbalimbali.
  1. MATUMIZI YA VIAMBISHI
Mtambaji hodari ana ufundi wa kutumia viashiria mbalimbali kukoleza usimulizi wake. Viashiria hivyo ni kama: -
  • Mikono
  • Mikunjo ya uso
  • Mchezesho wa macho
  • Viungo vingine vya mwili
  1. MATUMIZI YA WAKATI ULIOPO
Wakati uliopo kihistoria au uliopita kisimulizi.
  • Usimulizi huwa katika wakati uliopita lakini pia huchanganya sifa zinazohusisha wakati uliopo ilikuonesha umbali uliopo kati ya hadhira na simulizi umepunguzwa.
  1. UIGIZAJI
Msimulizi wa hadithi anaiga sauti mbalimbali za wahusika au wanyama katika utambaji wake.



Post a Comment

0 Comments